TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZIPATAZO 877 SERIKALINI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 877 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Mtendaji Halamashauri ya Wilaya ya Liwale, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Waajiri wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mkurugenzi wa Jiji Halmashauri ya Jiji la Tanga, Mkurugenzi wa Mji Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Ili kuona nafasi hizo za kazi zilizotangazwa tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz.
Imetolewa na Kitengo cha mawasiliano serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Juni, 2014.

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post