MAJINA MATANO BORA YALIYOPENDEKEZWA NA CCM KUWANIA NAFASI YA URAISI (KUTOKA DODOMA)


Taarifa ambazo zimethibitishwa kupitia mtandao wa twitter wa CCM na Rais Jakaya Kikwete zinasema kuwa, Kamati Kuu ya CCM imekamilisha kazi na kuwapitisha wagombea watano.
Wagombea waliopitishwa ni Bernard Membe, January Makamba, Dkt Asha Rose Migiro, Dkt John Magufuli na Balozi Amina Salum.
Majina haya yatapelekwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho kitakachoanza leo majira ya saa 4 asubuhi kwa ajili ya kupata majina matatu.
Katika hatua nyingine, wajumbe watatu wa kamati kuu Dkt Emmanuel Nchimbi, Sofia Simba na Adam Kimbisa wamepinga maamuzi hayo kwa madai ya ukiukwaji wa kanuni katika kuwapata wagombea hao watano kati ya 38 walioomba kuteuliwa.
Dkt Nchimbi amesema hawaungi mkono uteuzi huo sababu mojawapo ikiwa kuachwa kwa baadhi ya wagombea baada ya kikao cha kamati ya maadili kinyume cha katiba ya CCM.
 

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post