TANGAZO TOKA SERIKALINI KUHUSU USOMAJI WA STASHAHADA YA UALIMU KWA MIAKA MITATU KWA WALIOMALIZA FORM FOUR

TANGAZO MUHIMU TOKA
SERIKALINI
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO
KIDATO CHA TANO KWA TAHASUSI ZA
MASOMO YA SAYANSI, HISABATI, ENGLISH NA
UALIMU KWA MUDA WA MIAKA 3
UTANGULIZI
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inakaribisha maombi ya kujiunga na Masomo ya
Kidato cha Tano kwa tahasusi za masomo ya
Sayansi, Hisabati English, na Ualimu kwa muda
miaka 3 kwa wahitimu wa Kidato cha IV wenye
ufaulu wa Daraja la I hadi III kati ya mwaka
2004 na 2013. Katika masomo haya mwanafunzi
atasoma masomo ya Sekondari ya Kidato cha V
na VI na kufanya mtihani wa taifa wa Kidato cha
VI na kuendelea na Mafunzo ya Ualimu kwa
mwaka mwingine mmoja ambapo atatunukiwa
Stashahada ya Ualimu. Awali, mfumo huu
ulikuwa unajulikana kama half combination.
Nafasi hizi zinatolewa kutokana na upungufu
mkubwa wa walimu wa masomo ya Sayansi,
Hisabati na English katika shule za sekondari
nchini.
Masomo tajwa yataendeshwa katika vyuo
vifuatavyo: Butimba, Morogoro, Monduli,
Korogwe, Songea na Mpwapwa.
Tahasusi zitakazofundishwa ni kama ifuatavyo:
i.
Chemistry, Biology & Education (CBE)
ii.
Biology, English & Education (BEE)
iii.
Physics, English & Education (PEE)
iv.
Mathematics, English & Education (MEE)
v.
Chemistry, English & Education (CEE)
vi.
Chemistry, Mathematics, & Education (CME)
vii.
Nutrition, English & Education (NEE)
viii.
Agriculture, English & Education (AEE)
ix.
Biology, Nutrition & Education (BNE)
x.
Chemistry, Nutrition & Education (CNE)
xi.
Chemistry, Agriculture & Education (CAE)
xii.
Physics, Chemistry & Education (PCE)
xiii.
Geography, Mathematics, & Education (GME)
xiv.
Chemistry, Geography & Education (CGE)
xv.
Physics, Biology & Education (PBE)
xvi.
Physics, Mathematics & Education (PME)
MAELEZO MUHIMU
(i) Wale ambao tayari wameshatuma
maombi yao kwa masomo haya hawahitaji
kuomba tena kwani maombi yao
yanashugulikiwa
(ii) Majibu kwa watakaochaguliwa
kujiunga na mafunzo ya Ualimu yatatolewa
kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi ( www.moe.go.tz ), OWM-TAMISEMI
( www.pmoralg.go.tz ) na NACTE
( www.nacte.go.tz )
(iii) Waombaji watakaochaguliwa
watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na
Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa
wamepangwa kupitia anuani zao;
(iv) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya
Wizara: www.moe.go.tz , OWM
TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na
NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye
ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya
Ualimu.
VIAMBATISHO
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume
maombi yao kwa njia ya Barua
ikionyesha anuani kamili ya mwombaji , namba
ya simu, pamoja na Nakala ya Cheti cha ufaulu
wa Kidato cha IV.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 10
JULY 2014.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
7 MTAA WA MAGOGONI ( Zamani S.L.P.
9121) 11479 DAR ES SALAAM (Aione:
Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
Kwa wale walioko mikoani, maombi yanaweza
kupelekwa kwa Afisa Elimu wa Wilaya ambaye
atayawasilisha kwa Katibu Mkuu, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
DOWNLOAD PDF HAPA

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post