WATU 24 WAPOTEZA MAISHA KATIKA SHEREHE YA EID


Watu 24 wakanyagwa hadi kufa mjini Conakry Guinea
Takriban watu 24 wamekufa mjini Conakry Guinea baada ya umati kukanyagana katika sherehe ya kuadhimisha kukamilika kwa mfungo wa ramadhan.

24 waaga katika sherehe ya Eid
Watu wengine wengi walijeruhiwa ufukweni kandokando ya kitongoji cha Ratoma ambapo maelfu ya watu walikusanyika kusherehekea.
Shamra shamra hizo zilihudhuriwa na kundi la wanamziki la Instinct Killers ambao walikuwa kivutia kwa uma.
Utawala nchini humo umefunga fuo zote mjini Cananky na kumfuta kazi kiongozi wa shirika lililoandaa sherehe hizo.
Kumetangazwa pia wiki moja ya maombolezi.

SOURCE: BBC 

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post